Radio Maria Tanzania
                                
                                    
                                        
                                    
                                
                            
                            
                    
                                
                                
                                February 11, 2025 at 02:08 AM
                               
                            
                        
                            LEO FEBRUARI 11 TUNAMKUMBUKA MAMA YETU BIKIRA MARIA  WA LURDI (1858)
Miaka minne kisha kutangazwa
Nguzo ya Imani juu ya Bikira Maria Kukingiwa Dhambi ya Asili, yaani Mwaka 1858, msichana mmoja jina lake Bernadeta (tunayemkumbuka Aprili 15) alieneza habari kwa ujasiri kwamba Bikira Maria alimtokea mara nyingi.
Alimtokea huko Lurdi (Ufaransa) katika pango karibu ya mto Gave katika jimbo la Tarbe.
Miujiza mingi
ilifanyika hapo baadaye, Hii ilikuwa
ishara dhahiri kwa Mkristo yeyote kwamba 'mkono wa Mungu' ulionekana hapo. 
Katika pango hilo chemchemi 'ambayo haikujulikana hapo awali" ilijitokeza. Chemchemi hiyo imekuwa ndiyo sababu ya miujiza mingi.
Miujiza ambayo imeifanya Lurdi iudhihirishi zaidi umaarufu wake, wagonjwa hupona kwa kuyaoga maji hayo. 
Basi, watu walizieneza habari za miujiza iliyotendeka kwenye pango hilo. Siku hadi siku hiakundi makubwa ya watu walifika huko Lurdi. 
Kwa sababu hiyo Askofu wa Tarbe alifanya uchunguzi mahususi na baadaye ibada kwa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili iliruhusiwa kufanyika katika pango hilo. 
Mara akanisa lilijengwa mahali hapo.
Kwa njia ya binti huyu mdogo, Bikira Maria amewaita wadhambi wengi kutubu dhambi zao, na hivyo kukuza katika Kanisa moyo mkuu wa sala, ukarimu na upendo, hasa kwa maskini na wagonjwa.
Mwaka hata Mwaka Mahujaji kwa maelfu na maelfu hufika Lurdi na kwa jina la Bikira Maria, Mama yake, Mungu anaueneza utukufu wake kote duniani. 
Baadhi ya ibada zifanyikazo hapo ni maandamano pamoja na Sakramenti Takatifu; wagonjwa huomba afya kwa Mungu kwa maombezi ya Bikira Maria na wengi hupona mara moja. 
Papa Pius wa Kumi aliieneza sikukuu hii kwa Kanisa zima, kokote duniani.
BIKIRA MARIA WA LURDI UTUOMBEE.
                        
                    
                    
                    
                    
                    
                                    
                                        
                                            🙏
                                        
                                    
                                        
                                            ❤️
                                        
                                    
                                        
                                            👍
                                        
                                    
                                        
                                            👏
                                        
                                    
                                        
                                            💴
                                        
                                    
                                    
                                        60