CRDB Bank Plc
January 20, 2025 at 09:47 AM
Benki ya CRDB imetunukiwa tuzo 2 za 'Top Employer' kimataifa, ikithibitisha kuwa ni moja ya waajiri bora barani Afrika. Tuzo hizo zinatambua juhudi kubwa za benki katika kuweka mazingira bora ya kazi, kuwekeza kwenye vipaji na mafunzo, ujumuishi na usawa wa kijinsa, na kutoa fursa kwa wafanyakazi wake kukua na kuleta mabadiliko chanya.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Makao Makuu ya Benki jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Benki ya CRDB, Godfrey Rutasingwa amesema “Tuzo hii ni ishara ya wazi kwamba Benki yetu inajali na kuthamini wafanyakazi wake, ikiwapa mazingira bora yanayowezesha mafanikio yao binafsi na ya kitaaluma."
Kwa miaka mingi, Benki yetu imekuwa na dhamira thabiti ya kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na zana, usaidizi, na fursa zinazohitajika ili kufikia malengo yao ya kitaaluma. Tuzo hii ni ushuhuda wa mwendelezo wa Benki yetu kuwa 'Kitovu cha Ubora'. Mwaka jana Benki ilitunukiwa tuzo zaidi ya 50 katika nyanja mbalimbali.
Tunapojivunia mafanikio haya, tunawashukuru wafanyakazi wetu kwa bidii yao na kujitolea kwa moyo wote. Huu ni ushindi wa pamoja, na tunajivunia kuendelea kutoa mazingira bora ya kazi kwa wote.
#crdbbank
#topemployer
❤️
👍
🙏
😂
20