TCRA TANZANIA

TCRA TANZANIA

256.0K subscribers

Verified Channel
TCRA TANZANIA
TCRA TANZANIA
January 18, 2025 at 11:21 AM
Meneja wa Ofisi ya TCRA Kanda ya Kaskazini Mhandisi Francis Mihayo, akitoa elimu kwa umma kuhusu usalama mtandaoni, vilabu vya kidijiti na kuhamasisha usajili wa kikoa cha Taifa cha Dot TZ (.tz) katika kituo cha redio cha Shalom FM (97.3) Arusha, Januari 17, 2025. Elimu hii ni mwendelezo wa kampeni ya TCRA ya Ni Rahisi Sana, inayosisitiza matumizi ya mtandao yanayozingatia usalama ili kuepusha matukio ya utapeli na udukuzi, pamoja na matumizi ya namba 100, 15040 na *106# kwenye huduma za mawasiliano. Kampeni hii pia inalenga kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kikoa cha dot TZ (.tz ) kwenye huduma za intaneti, pamoja na umuhimu wa uanzishaji wa vilabu vya kidijiti kwa wanafunzi wa ngazi zote za elimu. #tcratz #nirahisisana #elimukwaumma #mtandaonifursabakisalama #dottzdomain #tzdimain #digitalclubs #klabuzakidijiti
👍 2

Comments