
TCRA TANZANIA
January 30, 2025 at 01:08 AM
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Ofisi ya Zanzibar, Bi. Esuvatie-Aisa Masinga akiwasilisha mada kwa kundi la watu wenye ulemavu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar kuhusu usalama mtandaoni kupitia kampeni ya “NI RAHISI SANA” tarehe 29 Januari, 2025, katika ukumbi wa ZSSF Michenzani Mall Zanzibar.
Meneja, akiwasilisha mada hiyo alisema TCRA inaendelea kukutana na kutoa elimu na kubadilishana uzoefu na makundi mbalimbali ya watumiaji wa huduma za mawasiliano kwenye jamii ili kujua namna bora ya kuwahudumia watu wenye ulemavu ili kufikia dira ya TCRA kuona jamii nzima iliyowezeshwa na huduma za mawasiliano. Semina hii imewafikia jumla ya washiriki 120 huu ni muendelezo wa semina nyingine zitakazo wafikia makundi mengine ya watu wenye mahitaji maalum.
📸👉https://www.instagram.com/p/DFbanrQPi9I/?img_index=1
#tcratz #elimukwaummama #uchumiwakidijiti #klabuzakidijiti #nirahisisanakuwasalamamtandaoni #nirahisisana
❤️
🙏
2