
TCRA TANZANIA
January 31, 2025 at 12:13 PM
📌 Usalama Mtandaoni na Watu wenye mahitaji Maalumu, Zanzibar
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Ofisi ya Zanzibar kwa ushirikiano na Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Zanzibar imeandaa semina maalumu ya usalama mtandaoni kupitia kampeni ya “NI RAHISI SANA” kwa kundi la watu wenye ulemavu tarehe 29 Januari, 2025, katika ukumbi wa ZSSF Michenzani Mall, Mjini Magharibi, Zanzibar.
Semina hiyo imeendeshwa na timu ya TCRA Zanzibar ikiongozwa na Meneja wa TCRA, Ofisi ya Zanzibar Bi. Esuvatie-Aisa Masinga.
#tcratz #elimukwaummama #uchumiwakidijiti #klabuzakidijiti #nirahisisanakuwasalamamtandaoni #nirahisisana #zanzibar
🙏
❤️
5