Bank of Tanzania

Bank of Tanzania

293.7K subscribers

Verified Channel
Bank of Tanzania
Bank of Tanzania
February 1, 2025 at 08:33 AM
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, amefungua kikao kazi kilichoandaliwa na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Airpay Tanzania chenye lengo la kuboresha utoaji wa mikopo kwa wananchi na urejeshaji kidijitali. Gavana Tutuba amesema urejeshaji huo wa mikopo kwa urahisi utatumia mfumo wa malipo uliotengenezwa na Airpay Tanzania ambao utaweza kutunza data na kubaini mlipaji mzuri na mbaya kwa hatua zaidi. Aidha, Gavana Tutuba ametoa wito kwa vikundi pamoja na watu wote wanaokopa fedha serikalini na kwenye mabenki kutumia fedha hizo vizuri na kuzirejesha kwa wakati ili wengine waweze kukopa pia. Washiriki wengine wa mkutano huo ni pamoja na mabenki, kampuni zinazotoa huduma ya mawasiliano ya simu za Tanzania Bara na Zanzibar. pamoja na Kampuni za kuchakata taarifa za mikopo (Credit Reference Bureau. https://www.instagram.com/p/DFgKxuyOxVe/?igsh=MWdlYzRkNDh6cWMzNg==
👍 ❤️ 😮 🇦🇴 🇹🇿 💀 13

Comments