
Bank of Tanzania
293.7K subscribers
Verified ChannelAbout Bank of Tanzania
Welcome to the Bank of Tanzania (BoT) channel, your go-to source for real-time updates and information about our services, policies, and initiatives.
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

SERIKALI YASAINI MIKATABA YA UNUNUZI NA USAFISHAJI DHAHABU Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesaini mikataba ya ununuzi na usafishaji dhahabu na kampuni za uchimbaji madini pamoja na Kiwanda cha Usafishaji Dhahabu cha Geita (GGR). Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo imefanyika leo, tarehe 16 Juni 2025, katika Ukumbi wa Kambarage uliopo Wizara ya Fedha jijini Dodoma, na kushuhudiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, pamoja na Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde. Dkt. Nchemba alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa Kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini, kinachowataka wachimbaji kuuza asilimia 20 ya uzalishaji kwenye masoko ya ndani, ikiwemo Benki Kuu yenye haki ya kwanza ya ununuzi wa dhahabu. Alisema hatua hiyo itaongeza akiba ya fedha za kigeni na kusaidia viwanda vya usafishaji dhahabu nchini kupata ithibati ya kimataifa ya LBMA. Alibainisha kuwa hadi sasa BoT imenunua tani 5 za dhahabu zenye thamani ya dola milioni 554, zaidi ya lengo la dola milioni 350 kwa mwaka 2024/25. “Hii ni hatua ya kihistoria kwa sababu inahakikisha dhahabu inasafishwa hapa nchini na kutunzwa kama sehemu ya akiba ya taifa,” alisema Dkt. Nchemba. Aliongeza kuwa lengo la BoT ni kununua tani 6 kwa mwaka wa fedha 2024/25, huku akitoa wito wa kuendeleza mkakati huu wa kitaifa kwa kuwa bei ya dhahabu imeendelea kupanda kimataifa. Naye, Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde, alisema mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 9.0 mwaka 2015 hadi 10.1 mwaka 2024/25. Mapato kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali yameongezeka kutoka Sh. bilioni 162 hadi Sh. bilioni 753, lengo likiwa ni kufikia Sh. trilioni 1. Kwa upande wake, Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, alisema mpango wa ununuzi wa dhahabu ulianza mwaka wa fedha 2022/23 ili kupunguza utegemezi wa mikopo ya nje na kuongeza akiba ya nchi ya fedha za kigeni. Makampuni ya Shanta Mining, Buckreef, Geita Gold Mining na Kiwanda cha Usafishaji Dhahabu cha Geita (GGR) yamesaini mikataba hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano na serikali katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini. https://www.instagram.com/p/DK-H2dWIYlM/?igsh=MXFodXplaXZwcjBpOQ==

Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tanzania, ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Gavana wa Benki Kuu, Bw. Emmanuel Tutuba, imefanya ziara katika mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma. Ziara hiyo imefanyika tarehe 17 Juni 2025, ambapo Msimamizi wa Mradi, Mhandisi Kedrick Chawe, alieleza kuwa mradi huo unatekelezwa chini ya usimamizi wa TANROADS kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Ujenzi huo unajumuisha njia ya kuruka na kutua ndege (runway), jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, pamoja na miundombinu mingine muhimu. Kukamilika kwa uwanja huu kunatarajiwa kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii, kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, kurahisisha usafirishaji wa mizigo, na hivyo kuongeza mapato ya serikali. Aidha, mradi huu utaimarisha hadhi ya Dodoma kama mji mkuu na kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa taifa. https://www.instagram.com/reel/DLCil3zO4RL/?igsh=MWYzbThydjd4NmRi

Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tanzania, ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Gavana wa Benki Kuu, Bw. Emmanuel Tutuba, imefanya ziara katika mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma. Ziara hiyo imefanyika tarehe 17 Juni 2025, ambapo Msimamizi wa Mradi, Mhandisi Kedrick Chawe, alieleza kuwa mradi huo unatekelezwa chini ya usimamizi wa TANROADS kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Ujenzi huo unajumuisha njia ya kuruka na kutua ndege (runway), jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, pamoja na miundombinu mingine muhimu. Kukamilika kwa uwanja huu kunatarajiwa kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii, kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, kurahisisha usafirishaji wa mizigo, na hivyo kuongeza mapato ya serikali. Aidha, mradi huu utaimarisha hadhi ya Dodoma kama mji mkuu na kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa taifa. Katika hatua nyingine, Bodi hiyo ilitembelea Kiwanda cha kutengeneza mvinyo wa zabibu cha CETAWICO kilichopo Hombolo, jijini Dodoma, ambako walipokelewa na Mkurugenzi wa Masuala ya Shirika, Bi. Katherine Mwimbe. Alieleza kuwa uwepo wa kiwanda hicho umeleta manufaa makubwa ya kiuchumi na kijamii, ikiwemo kuongeza kipato cha wakulima wadogo kwa kununua zabibu zao na kutoa ajira kwa zaidi ya watu 5,000 katika sekta ya kilimo kupitia zao la zabibu. Kiwanda cha CETAWICO kinachangia kutangaza bidhaa za Tanzania katika soko la kimataifa kupitia mauzo ya mvinyo bora, hivyo kuimarisha mnyororo wa thamani wa kilimo na kuchochea maendeleo ya viwanda nchini. Ziara hizo za Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tanzania katika miradi ya kimkakati na shughuli za kiuchumi zinawawezesha kupata uelewa wa kina kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo, changamoto zilizopo, na mchango wake katika kukuza uchumi wa taifa, ili kuwezesha maamuzi sahihi na yenye tija katika usimamizi wa sera ya fedha na maendeleo ya uchumi wa nchi. https://www.instagram.com/p/DLA36zCov9R/?img_index=5&igsh=dTloZmU4dDh3Ynlh