TCRA TANZANIA

TCRA TANZANIA

256.0K subscribers

Verified Channel
TCRA TANZANIA
TCRA TANZANIA
February 13, 2025 at 11:18 AM
Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof Palamagamba Kabudi (Mb.) akitoa hotuba katika mkutano wa mwaka wa vyombo ya utangazaji nchini unaofanyika jijini Dodoma. Kwenye hotuba yake Waziri Prof. Kabudi amesisitiza vyombo ya utangazaji kuwa na matumizi fasaha ya lugha ya Kiswahili ili kusaidia kukua kwa lugha hiyo. Prof. Kabudi amewataka Waandishi wa Habari kuandaa vipindi kwa kuzingatia weledi na ufasaha wa matamshi unaoenda sambamba na matumizi sahihi ya lugha na kuendelea kutumia taaluma ya Uandishi wa Habari kuandaa vipindi vyenye tija kwa jamii kuchochea maendeleo ya nchi. Mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji unafanyika kwa siku mbili jijini Dodoma na unaongozwa na kauli mbiu ya “Wajibu wa vyombo vya utangazaji kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025” #tcratz #abc2025 #broadcasting
❤️ 👍 😢 🙏 13

Comments