NMB Bank Plc
February 12, 2025 at 11:17 AM
Dar es Salaam 📍
Uwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Fedha la IFC ukiongozwa na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika anayehudumia Sekta ya Fedha, Ndugu Aliou Maiga, umetembelea makao makuu ya Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam na kukutana na uongozi wa benki yetu ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Bi. Ruth Zaipuna.
Katika mazungumzo yao, walikubaliana kuendeleza ushirikiano utakaoleta masuluhisho ya kifedha yanayokidhi mahitaji ya makundi mbalimbali nchini.
Kama benki, tutaendelea kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi katika kukuza uchumi wa nchi yetu.
#nmbkaribuyako
❤️
🙏
👍
👏
😂
😮
🥰
20