
NMB Bank Plc
February 13, 2025 at 06:28 PM
Pwani 📍
Kama mdau wa Sekta ya Elimu nchini, tunaendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha sekta hii ili kujenga Taifa bora la kesho.
Kupitia Sera yetu ya kurejesha kwenye jamii (CSI), tumekabidhi mabati 400 yenye thamani ya Shilingi Milioni 16 kwa shule za Wilaya ya Kisarawe za :
➡️ Sekondari ya Suleiman Jafo
➡️ Sekondari ya Jokate Mwegelo
➡️ Sekondari ya Kisangile
Msaada huu umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti na uwakilishi wa benki umeongozwa na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio.
#nmbkaribuyako
🙏
👍
❤️
🇹🇿
😮
14