
Dimbani Konekti
January 23, 2025 at 07:38 AM
Manchester City wako hatarini kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchezea kichapo cha mabao 4-2 dhidi ya Paris Saint-Germain.
Ikumbukwe katika mfumo mpya wa timu 36, timu zinazomaliza nafasi ya 25 au chini haziingii hatua nyingine wala kwenda Europa League,
City wako nafasi ya 25 na wanahitaji ushindi dhidi ya Club Brugge wiki ijayo pamoja na kuziombea mabaya timu za juu yao kutochukua ushindi ili kusonga mbele.
Katika mechi dhidi ya PSG, licha ya kuongoza 2-0 kupitia Jack Grealish na Erling Haaland, City walipoteza baada ya mabao ya Ousmane Dembele, Bradley Barcola, Joao Neves, na Goncalo Ramos wa PSG.
😂
❤️
👍
😮
🙏
😢
☠️
🇹🇿
54