
Dimbani Konekti
January 26, 2025 at 02:38 PM
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford (27), ameonesha nia na utayari wake kuihama klabu hiyo yenye maskani yake jijini Manchester Uingereza akitaka kujiunga na Barcelona ya nchini Hispania.
Akiweka wazi yupo tayari kupunguziwa mshahara ili kujiunga na Watacalunya hao kutoka kwa mashetani wekundu wa Manchester, huku ikiripotiwa mshambuliaji huyo kuzipiga chini ofa kadhaa za vilabu kutoka Saudi Arabia na kuongeza msisitizo kwenye nia yake ya kujiunga na Barca.
👍
❤️
😂
😮
😢
🙏
👏
26