Dimbani Konekti

Dimbani Konekti

206.5K subscribers

Verified Channel
Dimbani Konekti
Dimbani Konekti
February 13, 2025 at 09:06 AM
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesogeza mbele mchezo baina ya Simba na Dodoma Jiji FC ambao ratiba ya awali inaonyesha ulipangwa kuchezwa Februari 15, 2025 katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Kuahirishwa kwa mchezo huo kumekuja ikiwa ni siku mbili tangu msafara wa Dodoma Jiji ulipopata ajali katika eneo la Somanga, Kilwa, Lindi wakati ulipokuwa ukija Dar es Salaam ukitokea Ruangwa, Lindi ambako timu hiyo ilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC, Jumapili, Februari 9, 2025 ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2. Taarifa ya TPLB leo imesema kuwa mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine. “BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeahirisha mchezo namba 148 wa Ligi Kuu ya NBC (Simba SC vs Dodoma Jiji) ambao ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa KMC Complex Februari 15, 2025 kuanzia saa 10:00 alasiri. Sababu ya kuahirishwa kwa mchezo huo ni baadhi ya wachezaji na maofisa wa ufundi wa klabu ya Dodoma Jiji kutokuwa katika hali nzuri kiafya baada ya basi la klabu hiyo walilokuwa wakisafiria kutoka Ruang
👍 😢 ❤️ 🙏 🇹🇿 👏 😂 😭 😮 😻 46

Comments