
Wizara ya Afya Tanzania
February 9, 2025 at 06:03 PM
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu baada ya kuwasili kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Malawi leo Februali 9, 2025 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 74 wa Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Afya ya nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (ECSA-HC) unaotarajia kufanyika kuanzia tarehe 10 hadi 12 Februali, 2025 katika mji wa Lilongwe nchini humo.
Waziri Mhagama ameambatana na ujumbe wake kutoka nchini Tanzania akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe pamoja na Mshauri wa Rais katika masuala ya afya na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohammed Janabi.
🙏
😢
3