Wizara ya Afya Tanzania WhatsApp Channel

Wizara ya Afya Tanzania

230.4K subscribers

Verified Channel

About Wizara ya Afya Tanzania

Karibu kwenye ukurasa rasmi wa Wizara ya Afya Tanzania katika mtandao wa Whatsapp. Fuatilia ukurasa huu kwa habari mbalimbali za Sekta ya Afya #tunaboreshaafya #afyanimtaji

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 12:59:22 PM

WAZIRI MHAGAMA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ametekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutembelea majeruhi wa ajali ya gari iliyotokea Meatu Mkoani Simiyu waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda BUGANDO Mkoani Mwanza ambao wanaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu ya awali. Waziri Mhagama ametekeleza maelekezo hayo leo Juni 17, 2025 kwa haraka ambapo amewajulia hali majeruhi hao pamoja na kutoa maelekezo kuwa wagonjwa hao (watano) watatibiwa kwa gharama za Serikali.

Post image
πŸ₯Ή πŸ˜‚ 3
Image
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 7:57:09 AM

WAMILIKI NA WATAALAMU WA MAABARA BINAFSI ZA AFYA WAHIMIZWA KUTOA HUDUMA KWA KUFUATA TAALUMA NA MAADILI. Wataalamu wa Maabara za Afya wametakiwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni zinazosimamia uendeshwaji wa Maabara hizo ili kutoa huduma bora kwa jamii. Hayo yamesemwa Juni 16,2025 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya wakati wa mkutano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wamiliki wa Maabara Binafsi za Afya na wataalamu wa Maabara uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa jijini Dodoma. Amesema wataalamu wa maabara ni wadau muhimu kwani wanafanya kazi kwa kushirikiana na Madaktari ilikuweza kutambua magonjwa mbalimbali kwa kufanya vipimo na kutoa majibu sahihi kwa wagonjwa na sio vinginevyo. β€œLengo la maabara ni uchunguzi kulingana na maelezo ya mgonjwa na sio kufuta mapato/maslahi, kwa mfano mtu anasema anaumwa mguu huku unampima UTI kwasababu unamaslahi labda ya dawa au maelekezo mengine ya kimapato hivyo sio maadili ya kazi yako.” Amesema Bw. Mmuya Amewataka pia wanataaluma kukaa kwenye taaluma na kuifanyia kazi miiko ya taaluma yao. Aidha amesisitiza kuwa kila mtumishi afanye kazi kwa kufuata taaluma aliyoisomea ili kuweza kutoa huduma nzuri na yenye viwango kwa wananchi. β€œ Wagonjwa wakifika hospitalini hawajui nani ni nani wakiona tu umevaa koti jeupe wanajua ni daktari, sasa baadhi ya wanataaluma wa Maabara wanauvaa uhusika wa udaktari wakati wanajua sio madaktari hivyo nawasihi mfanye kazi kwa taaluma mliyosomea” amesema Bw. Mmuya Aidha Bw. Mmuya ametoa rai kwa wamiliki wa Maabara binafsi kuhakikisha Maabara zinakuwa na vitu vyote muhimu kulingana na miongozo inavyohitaji. β€œMajengo yawe na sifa za kutoa huduma husika, kulingana na miongozo, hii itasaidia kutoa huduma bora na mazingira mazuri lakini kinyume chake kutaleta shida kwa wagonjwa wakati wa kupata huduma.” amesema Bw. Mmuya Naye mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Thomas Rutachunzibwa amewaasa watendaji wa maabara kuhakikisha wanatoa majibu sahihi na kufuata miiko ya kazi.

Post image
❀️ πŸ‘ ❀ 😒 😌 20
Image
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 12:59:43 PM
Post image
πŸ˜‰ 1
Image
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 12:59:42 PM
Post image
Image
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 5:09:48 AM
Post image
πŸ‘ πŸ₯° ❀️ 🀝 6
Image
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 12:59:43 PM
Post image
πŸ‘ 2
Image
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 5:02:36 PM

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wabobezi wa darasa la uuguzi kwenye ngazi ya watoto waliotokana na 'Samia Scholaship Fund', kushoto ni Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daud Msasi na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Bahati Wajanga.

Post image
πŸ‘ πŸ˜‚ 🀝 4
Image
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 12:59:44 PM
Post image
πŸ‘ 2
Image
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 5:10:31 AM

KUJENGEWA UWEZO MADAKTARI NA WATOA HUDUMA MKOANI GEITA KUTAONGEZA UFANISINA UBORA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA Na WAF - GEITA Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Geita Hermani Matemu amesema licha ya wananchi wa Mkoa huo kunufaika na Huduma za kibingwa kwa ukaribu na kwa gharama nafuu lakini pia kujengewa uwezo kwa wataalamu na watoa huduma katika mkoa huo kutasaidia kuzidi kuimarika kwa hali ya utoaji na Ubora wa huduma kwenda sambamba na nia ya Mhe. Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora. Bw. Matemu ameyasema hayo Julai 16, Mkoani Geita wakati wa Mapokezi ya Madaktari bingwa wa Rais Samia ambao watakua mkoani hapo kwa Muda siku 7 kutoa huduma za Afya kibingwa Mkoani hapo. β€œWananchi wetu watapata kile ambacho wanakitaka, mtaweza kuwajengea wataalamu ili baada ya nyie kuondika wananchi waendelee kupata huduma na itasaidia japokua itakua sio kwa kiwango kile mnachotoa nyinyi lakini tija itakuwepo” amesema Matemu. Nae Mratibu wa zoezi la Madaktari bingwa wa Rais Samia kwa mkoa wa Geita Paskalina Endrew kutoka wizara ya afya amesema lengu kuu la zoezi hili kuwasogezea wananchi huduma za kibingwa na bobezi na kuwajengea uwezo watoa huduma katika maeneo yao ya kazi. Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Geita Dkt. Stephen Mwaisobwa pamoja na Dkt. Neveline Mwakaboko mganga mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale wamewataka wananchi wenye uhitaji wa matibabu ya kibingwa kujitokeza kwenye hosptali za wilaya zilizopo kila halmashauri ili kupata huduma ya matibabu.

Post image
❀️ πŸ™ 3
Image
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
6/17/2025, 5:09:47 AM

βΈ» MIKOA, WILAYA KUENDELEA KUIMARISHWA ILI KUSIMAMIA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII Na WAF, Lindi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dkt. Kheri Kagya, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha zaidi uwezo wa mikoa na halmashauri katika kusimamia na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa kazi za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) ili kuhakikisha huduma bora na zenye ufanisi zinafika moja kwa moja kwa wananchi. Dkt. Kagya ameyasema hayo leo Juni 16, 2025, alipokutana na timu ya wataalam kutoka Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais – TAMISEMI waliofika ofisini kwake kwa ajili ya zoezi la Usimamizi Shirikishi wa Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii mkoani humo. Ameeleza kuwa jitihada za Serikali za kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji na usimamizi wa CHW zinatoa fursa kwa timu za mikoa na halmashauri kuhakikisha kuwa huduma zinatolewa kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Afya na mahitaji halisi ya jamii. β€œTunapongeza hatua hizi za kuimarisha ufuatiliaji na tunaamini kuwa kuziwezesha timu za mikoa na halmashauri kutafanikisha usimamizi bora hadi ngazi za vitongoji na mitaa ambako CHW wanatumikia jamii zao,” amesema Dkt. Kagya. Ameongeza kuwa mkoa wa Lindi kupitia halmashauri zake ikiwemo Lindi Manispaa, Mtama, na Ruangwa, umefanikiwa kutoa mafunzo kwa idadi kubwa ya CHW katika vyuo vya afya vilivyopo mkoani Lindi na Mtwara, hatua inayochochea uboreshaji wa huduma za afya ngazi ya jamii. Kwa upande wake, kiongozi wa msafara kutoka Wizara ya Afya, Bi. Orsolina Tolage, ameeleza kuwa lengo la zoezi la usimamizi shirikishi ni kuhakikisha mpango unatekelezwa kwa ufanisi na huduma zinazotolewa na CHW zinaboresha afya za wananchi. Amebainisha kuwa mafunzo ya awamu ya kwanza kwa CHW mkoani humo yalianza Oktoba 2024 na kukamilika Aprili 2025, na kwamba timu hiyo inakusanya taarifa za kina ili kuwa na kanzi data sahihi ya waliohitimu na wanaoendelea na mafunzo.

Post image
πŸ‘ 1
Image
Link copied to clipboard!