Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

230.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
February 10, 2025 at 09:53 AM
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye Mkutano wa 74 wa Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (The East, Central and Southern Africa Health Community - ECSA-HC) unaofanyika Lilongwe nchini Malawi kujadiliana masuala ya afya wanachama wa Jumuiya hiyo. Mkutano huo umefunguliwa rasmi leo Februari 10, 2025 na Makamu wa Rais wa Malawi Dkt. Michael Bizwick Usi na kuwakutanisha kwa pamoja Viongozi na wataalam wa Sekta ya Afya kutoka nchini tisa wanachama wa Jumuiya hiyo. Jumuiya ya ECSA-HC barani Afrika inajumuisha nchi za Tanzania, Malawi, Kenya, Lesotho, Zambia, Zimbabwe, Mauritius, Uganda pamoja na Eswatini.
🙏 ❤️ 😢 4

Comments