Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

231.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
February 13, 2025 at 08:19 AM
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya Mawaziri wa Afya alipowasili katika Mkutano wa Tatu wa mwaka wa Programu ya Viongozi ambao ni mwendelezo wa utekelezaji wa jitihada za makusudi za Africa CDC ili kujenga uelewa wa pamoja miongoni mwa Mawaziri wa Afya wa Afrika. Mkutano huo unaofanyika leo Februari 13, 2025 jijini Addis Ababa, Ethiopia, unakusudia pia kusisitiza msimamo wa uongozi katika kufanikisha malengo ya Mpango Mkakati wa Africa CDC 2023 hadi 2027 pamoja na Mpango wa Afya. Waziri Mhagama ameambatana pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC) Dkt. Ntuli Kapologwe, Mshauri wa Rais wa Tanzania katika masuala ya Afya na Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohammed Janabi, Mkurugenzi wa Huduma za Afya Mama na Mtoto Dkt. Ahmad Makuwani pamoja na wataalam wengine kutoka Wizara ya Afya.
👍 😢 🙏 ❤️ 👏 8

Comments