Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

231.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
February 14, 2025 at 07:33 AM
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Februali 13, 2025 ameshiriki kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Bidhaa 24 za Kipaumbele za Matibabu ya Afya pamoja na Dira ya utekelezaji wa kikanda kuhusu uzalishaji wa bidhaa za afya Afrika. Uzinduzi huo umefanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Muungano wa Afrika ya masuala ya Afya, African Union Development Agency (AUDA - NEPAD) unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya kupata huduma za afya kwa wote (UHC). Waziri Mhagama katika Mkutano huo ameambatana pua na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC) Dkt. Ntuli Kapologwe pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Afya ya Uzazi Mama na Mtoto Dkt. Ahmad Makuwani.

Comments