WIZARA YA MAMBO YA NJE

WIZARA YA MAMBO YA NJE

162.9K subscribers

Verified Channel
WIZARA YA MAMBO YA NJE
WIZARA YA MAMBO YA NJE
January 27, 2025 at 03:38 AM
Makamu wa Rais wa Gambia awasili Tanzania Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Gambia, Mhe. Muhammad Jallow amewasili jijini Dar es Salaam ambapo anamwakilisha Mheshimiwa Rais Adama Barrow katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaotarajiwa kuanza leo, Januari 27 na 28 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unawakutanisha viongozi wa nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo. Lengo ni kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalodhamiria kuimarisha juhudi za pamoja za Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika katika kuhakikisha Afrika inaondokana na changamoto za upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu. Mhe. Jallow amepokelewa na Waziri wa Maji nchini, Mhe. Jumaa Aweso.
👍 ❤️ 😂 😮 8

Comments