
WIZARA YA MAMBO YA NJE
January 28, 2025 at 09:59 AM
Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan, amewasili jijini Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Cosato Chumi, alimkaribisha Mheshimiwa Al Nahyan katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Al Nahyan ni miongoni mwa wageni waalikwa walioko nchini kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati.
Mkutano huo ulianza tarehe 27 Januari kwa majadiliano ya ngazi ya mawaziri, na tarehe 28 Januari,2025 Wakuu wa Nchi wanakutana kuhitimisha mkutano huo.
Aidha, mkutano huo unatarajiwa kupitisha Azimio la Dar es Salaam, ambalo linasisitiza dhamira ya pamoja ya viongozi wa Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu barani Afrika ili kuunga mkono maendeleo ya bara hili.
❤️
😢
👍
😮
🙏
9