WIZARA YA MAMBO YA NJE

WIZARA YA MAMBO YA NJE

162.9K subscribers

Verified Channel
WIZARA YA MAMBO YA NJE
WIZARA YA MAMBO YA NJE
January 30, 2025 at 08:45 PM
NAIBU WAZIRI CHUMI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA INDIA Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amekutana na kuzungumza na Balozi wa India nchini, Mhe. Shri Bishwadip Dey katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Wanadiplomasia hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India na jinsi ya kuendelea kuimarisha ushirikiano huo . Mhe. Chumi amemshukuru Balozi Dey kwa Serikali ya India kwa kuendelea kushirikiana kwa dhati na Tanzania na kuongeza kuwa ushirikiano thabiti na imara uliojengwa kwa muda mrefu kupitia sekta za Afya, Kilimo, Biashara na Elimu. Alieleza dhamira ya serikali ya Tanzania kuhusu mustakabali wa uhusiano wa Tanzania na India na kuahidi kuendelea kushirikiana kupitia miradi shirikishi ambayo inaweza kuleta manufaa kwa mataifa yote mawili kupitia sekta za kipaumbele kama vile kilimo ambapo mbinu bunifu zinaweza kutumika kuongeza usalama wa chakula. Aliongeza kuwa ushirikiano huo unaweza kuboresha mifumo ya utoaji huduma za afya, Elimu, biashara na viwanda kwa manufaa ya pande zote mbili. Mhe. Chumi pia alibainisha kuwa Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji zinazopatikana nchini na kumsihi Balozi huyo kutangaza fursa zilizopo nchini. Kwa upande wake Mhe. Balozi Dey aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kufanikisha mkutano wa Nishati Afrika “Mission300”. Aidha, Alibainisha kuwa Serikali ya India itaendelea kuunga mkono mipango ya maendeleo ya Tanzania na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano katika maeneo muhimu kama ya Viwanda, Elimu, Teknolojia, Biashara na Nishati. Mhe. Balozi Dey alisisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia ya kisasa ya akili mnemba katika sekta mbalimbali na kuongeza kuwa mbinu hii sio tu itakuza ukuaji wa uchumi bali pia itasaidia maendeleo endelevu kwa kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi na uwajibikaji.
❤️ 👍 😢 🙏 😂 11

Comments