WIZARA YA MAMBO YA NJE

WIZARA YA MAMBO YA NJE

160.1K subscribers

Verified Channel
WIZARA YA MAMBO YA NJE
WIZARA YA MAMBO YA NJE
February 6, 2025 at 11:45 PM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Palamagamba Kabudi amempokea Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Deng Kuol ambaye amewasili nchini Tanzania kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika Februari 7, 2025.
 Mkutano huu unautangulia Mkutano wa Dharura wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC utakaofanyika tarehe Februari 8, 2025. Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
❤️ 😮 2

Comments