
WIZARA YA MAMBO YA NJE
February 7, 2025 at 02:56 AM
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Denis Londo (Mb.) amempokea Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Wycliffe Mudavadi, ambaye amewasili nchini Tanzania kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika Februari 7, 2025.
Mkutano huu unautangulia Mkutano wa Dharura wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC utakaofanyika tarehe Februari 8, 2025.
Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi kuhusu hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
❤️
😂
👍
🙏
😢
17