JamiiCheck
                                
                                    
                                        
                                    
                                
                            
                            
                    
                                
                                
                                January 17, 2025 at 03:47 PM
                               
                            
                        
                            Wadau wa JamiiCheck.com wameshiriki Kuthibitisha picha mbili ambapo baadhi wamebainisha kuwa zote zimetengenezwa kwa kutumia Teknolojia ya Akili Mnemba (AI). 
Aidha, JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa yanayodhihirisha kuwa picha hizo si Halisi. Katika picha ya kwanza, mwanamke anaonekana na nywele zilizosukwa tofauti kati ya upande wa mbele na nyuma, huku kiganja kimoja kikionekana kubebana na kingine ambacho mkono hauonekani.
Picha ya pili inaonesha watu wawili walioungana isivyo kawaida walipokaa, huku mmoja akiwa na umbo la miguu lisilo halisi, miguu isiyoendana na mwili, na rangi tofauti za suruali kwa miguu yote miwili.
Soma https://jamii.app/ChallengeAI
                        
                    
                    
                    
                    
                    
                                    
                                        
                                            👍
                                        
                                    
                                        
                                            😂
                                        
                                    
                                        
                                            🙏
                                        
                                    
                                    
                                        3