
JamiiCheck
79.6K subscribers
Verified ChannelAbout JamiiCheck
A citizen-centered approach in countering Misinformation and Disinformation Online and Offline by JamiiForums
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Kusema Ukweli kila wakati huimarisha uaminifu na huchochea uwepo wa Taarifa Sahihi zitakazoiwezesha Jamii kufanya maamuzi sahihi. Ukweli hauhitaji kufichwa au kurekebishwa. Tembelea Jukwaa la JamiiCheck.com ili kupata Taarifa zilizohakikiwa sambamba na msaada wa Uthibitishaji wa maudhui yanayokupa mashaka juu ya Uhalisia wake.


JamiiCheck imefuatilia Uhalisia wa Picha za Boniface Mwangi zilizosambazwa Mtandaoni zikimuonesha akiwa na majeraha zikidaiwa kuwa ni za tukio la Mei 22, 2025 na kubaini kuwa ni Upotoshaji. Kwa kutumia nyenzo ya Kimtandao ya TinEye, JamiiCheck imejiridhisha kuwa picha hizo zilichapishwa na Mwangi Aprili 21, 2025 katika mtandao wake wa X akielezea tukio la kushambuliwa kwake na aliowataja kuwa ni Polisi wa Nairobi. Soma https://jamii.app/MwangiKujeruhiwa


JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa iliyochapishwa mtandao wa X ikidai Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima, ameituhumu CHADEMA kuhusika na mauaji ya Ali Kibao Si ya Kweli. Kupitia utafutaji wa maneno muhimu na marejeo ya video ya mkutano wa Askofu Gwajima Mei 24, 2025, hakutaja chama hicho kuhusika bali alikemea vitendo vya utekaji, akitumia tukio la Ali Kibao kama mfano. Aidha, chapisho lililotumika kusambaza taarifa hiyo limebainika kuwa la kughushi na halikutolewa na Millard Ayo. Soma https://jamii.app/GwajimaMatukioUtekaji


Mapambano dhidi ya Upotoshaji yanatuhitaji kutafuta na kuuweka wazi Uhalisia ili kuepuka Taarifa zisizo za Kweli katika Jamii. Maamuzi Sahihi huchochewa na Taarifa Sahihi. Wasambazie jamaa na marafiki ujumbe huu ili wainuke kupambana dhidi ya Taarifa Potofu. Soma https://jamii.app/PotoshiMaamuziMabovu


Kumbuka si kila Taarifa unayokutana nayo mtandaoni ni ya Kweli. Thibitisha kabla ya kuiamini na kuisambaza, kwani utaiweka jamii kuwa salama dhidi ya Taarifa Potofu. Unaweza kuwasilisha Taarifa inayokupa mashaka katika jukwaa la JamiiCheck.com ili kupata msaada wa Uhakiki. Soma https://jamii.app/ZuiaTaarifaPotofu


Taarifa zinazodai kuwa Dawa za Asili hazina Kemikali na kwamba ni salama kwa Asilimia 100 Si za Kweli Kupitia Tafiti na Machapisho ya kitaaluma, JamiiCheck imebaini kuwa dawa zote zina Kemikali hata zile za Asili ambazo huwa na Kemikali asilia kutoka kwa mimea na wanyama. Kemikali hizi zinaweza kuwa na athari chanya au hasi kwa afya ya binadamu. Mathalani Tanin inayopatikana kwenye baadhi ya mimea ina uwezo wa kuponya majeraha lakini pia inaweza kupelekea mwili kushindwa kufyonza Madini ya Chuma kama itatumika kwa kiwango kikubwa. Soma https://jamii.app/DawaZaAsili


Kupitia utafutaji wa maneno muhimu na marejeo ya video ya hotuba ya John Heche ya Mei 23, 2025, JamiiCheck imebaini na kujiridhisha kuwa Taarifa inayodai CHADEMA wameandika barua kwa Tume Huru ya Uchaguzi kuomba mazungumzo Si ya Kweli. Chapisho lililosambazwa pia Si la Kweli kwani halikutolewa na The Chanzo bali limetengenezwa na wapotoshaji. Katika kikao hicho cha Kamati Kuu ya CHADEMA, Heche alisisitiza msimamo wa "No reforms, No election" akitaja dosari za uchaguzi zinazohitaji ufumbuzi. Soma https://jamii.app/HecheMazungumzoNaTume


Kwa utafutaji wa kutumia maneno muhimu na marejeo ya video ya mkutano wa Askofu Gwajima Mei 24, 2025, JamiiCheck imejiridhisha kuwa Taarifa inayosambazwa kuwa Gwajima aliwatuhumu vijana wa CHADEMA kuhusika na shambulio dhidi ya Padri Charles Kitima Si ya Kweli. Aidha, Chapisho lililotumika kusambaza Taarifa hiyo ni la kughushi na halijatolewa na Jambo TV. Gwajima hakuwatuhumu vijana wa CHADEMA, bali alitoa wito wa kukomesha vitendo vya utekaji, akilitaja tukio la Padri Kitima kama mfano wa matukio yanayopaswa kushughulikiwa. Soma https://jamii.app/GwajimaTukioKitima


Ipo Taarifa inayosambazwa Facebook ikidaiwa kuchapishwa na Millard Ayo ikisema 'Sugu kujiunga rasmi CHAUMMA' Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu umebaini kuwa Taarifa hiyo haikuchapishwa na Millard Ayo kwenye kurasa zake rasmi za Mitandao ya Kijamii. Kumbuka wapotoshaji huweza kutengeneza chapisho wakitumia utambulisho wa chanzo fulani ili Kupotosha. Hakikisha Unathibitisha kabla ya kusambaza. Soma https://jamii.app/SuguKuhamiaChaumma
