
JamiiCheck
January 23, 2025 at 11:04 AM
Kumekuwepo na video inayomuonesha Rais wa Marekani, Donald Trump, akihutubia baada ya kuapishwa, ambapo anadaiwa kutambua uwepo wa Rigathi Gachagua na kutoa onyo kwa Rais wa Kenya, William Ruto, kuhusu matukio ya utekaji.
Ufuatiliaji wa kimtandao wa JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa kutoka kwenye video halisi iliyochapishwa na Sky News kwenye YouTube, ambapo Trump hakutoa kauli hiyo.
Video hiyo Imehaririwa kwa kuwekewa sauti iliyotengenezwa kwa Akili Mnemba pamoja na mchanganyiko wa sauti Halisi. Aidha, Gachagua hakuwepo kwenye hafla ya uapisho huo.
Soma https://jamii.app/VideoGachaguaNaTrump
❤️
🇹🇿
👍
😮
🙏
5