
JamiiCheck
January 23, 2025 at 04:06 PM
Wadau wa JamiiCheck walishiriki kuthibitisha video iliyomuonesha Rais Donald Trump akiongozana na kijana mrefu isivyo kawaida, wakibainisha kuwa ni ya kutengenezwa
Ufuatiliaji wa JamiiCheck ulibaini kuwa video hiyo ilipotoshwa kwa kuondoa picha halisi ya mtoto wa Trump, Barron Trump na kuweka picha iliyotengenezwa inayomuonesha kijana huyo akiwa mrefu kupita kawaida kiasi cha kuzidi usawa wa mlango.
Kadhalika mapungufu kadhaa yalibainika, kama vile viatu vya kijana huyo kuonekana kuelea na mtikisiko wa kuteleza. Kivuli cha viatu kisicholingana na mwanga wa nyuma, na kukatika kwa video pale anapofikia mlango, bila kuonesha aliingiaje ndani.
Soma https://jamii.app/MtuMrefuVideoTrump
👍
🙏
4