
JamiiCheck
January 25, 2025 at 11:34 AM
Licha ya asali kuwa na manufaa makubwa ikiwemo kutumika kama dawa ya baadhi ya magonjwa mathalani kutibu vidonda na kikohozi, lakini si salama kwa mtoto mwenye umri chini ya mwaka mmoja kwani husababisha tatizo liitwalo Infant Botulism.
Asali hubeba Bakteria jamii ya Clostridium Botulinum ambao si wazuri hivyo ni hatari kwa watoto kwa kuwa mifumo yao ya kinga pamoja na ya chakula inakuwa haijakomaa vizuri kuweza kuwaharibu iwapo atawala.
Kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa cha Marekani (CDC) hushauri Watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja wasipewe asali kama sehemu ya kuwakinga.
Soma https://jamii.app/AsaliMtotoMchanga
👍
❤️
😂
🏳️🌈
😢
🙏
13