JamiiCheck

JamiiCheck

83.3K subscribers

Verified Channel
JamiiCheck
JamiiCheck
January 26, 2025 at 04:36 PM
Kumekuwapo na Taarifa inayoonesha Freeman Mbowe aliandika kupitia Akaunti yake ya Mtandao wa X kuonesha nia ya kutaka kukata rufaa mara baada ya kushauriana na familia yake dhidi ya Matokeo ya uchaguzi wa CHADEMA yaliyomtangaza Tundu Lissu kuchukua nafasi yake. Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini Taarifa hiyo Si ya Kweli kwani Mbowe hakuchapisha Taarifa yoyote yenye nia ya kutaka kukata rufaa katika ukurasa wa Mtandao wa X wala Mitandao mingine ya kijamii. Aidha, Januari 22, 2024, ambayo ni tarehe inayoonekana katika chapisho hilo bandia, Mbowe aliandika ujumbe wa kukubali maamuzi yaliyofanywa katika uchaguzi wa mkutano mkuu wa CHADEMA huku akimpongeza Tundu Lissu kwa kuaminiwa na wapiga kura wa chama hicho kuwa Mwenyekiti wao Soma https://jamii.app/MboweKukataRufaa
🙏 1

Comments