JamiiCheck

JamiiCheck

79.6K subscribers

Verified Channel
JamiiCheck
JamiiCheck
January 28, 2025 at 11:30 AM
Kumekuwapo na Taarifa katika Mtandao wa YouTube zinazoeleza kuwa Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré amewasili Tanzania kushiriki Mkutano wa Nishati unaowakutanisha viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika unaofanyika Januari 27-28, 2025. JamiiCheck imefuatilia Taarifa hizo na kubaini kuwa Si za Kweli kwani Wachapishaji wameweka vichwa vya Taarifa ambavyo ni tofauti na Maudhui yaliomo kwenye Video hizo. Aidha, Idara ya Mawasiliano ya Rais wa Burkina Faso walieleza kuwa Januari 27, 2025, Captain Traoré alikuwa na kikao na Mawaziri wa Shirikisho la Sahel nchini humo kujadili mustakabali wao wa kujitoa ECOWAS na pamoja na ushirikiano wao. Soma: https://jamii.app/IbrahimMkutanoNishati
👍 ❤️ 💐 🙏 6

Comments