TheChanzo

TheChanzo

37.5K subscribers

Verified Channel
TheChanzo
TheChanzo
February 2, 2025 at 01:17 PM
*Mgogoro wa DR Congo Unaochochewa na Rwanda na M23 Kuwa Vita Kamili?* Waasi wa M23 wanaowezeshwa na Rwanda wameweza kuushika mji mkubwa wa Goma kwa mara ya pili toka mwaka 2013 walivyofurumishwa na kutoka katika mji huo. Kwa mwaka 2013, waasi hao walioushika Goma kwa mwaka mmoja, waling’olewa na kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa kilichokuwa kikiongozwa na aliyekuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la Tanzania, Luteni Jenerali James Aloizi Mwakibolwa.Operesheni hiyo maalum ilichukua miezi mitatu, na kuacha M23 wakikimbilia Rwanda na Uganda. Kwa wafuatiliaji wa mgogoro huu, kukamatwa kwa Goma sio jambo la kushangaza. Kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2024, kikundi cha M23 kikisaidiwa moja kwa moja na Rwanda,kiliweza kukamata maeneo mengi kwa kasi katika eneo la Kivu Kaskazini. Kuanzia kipindi hicho, eneo aliloshika M23 likawa ni kubwa zaidi kuwahi kutokea. Soma zaidi>>>https://thechanzo.com/2025/02/02/mgogoro-wa-dr-congo-unaochochewa-na-rwanda-na-m23-kuwa-vita-kamili/
👍 🕖 😢 🙏 4

Comments