
Ikulu Zanzibar
February 15, 2025 at 05:05 PM
RAIS MWINYI:TUHAMASISHE WANA CCM WAJITOKEZE KUPIGA KURA KWA WINGI
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezisisitiza Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi kuwahamasisha Wanachama na Wananchi kujiandikisha na kujitokeza kwa Wingi kupiga Kura ili CCM ishinde kwa Kishindo.
Dkt. Mwinyi ambae ni Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM ameyasema hayo alipozungumza na Wanachama na Wananchi Mauwani, Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba Katika Mkutano Maalum wa Mapokezi yake baada ya Kuteuliwa hivi Karibuni kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar.
Dkt.Mwinyi amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wana CCM kutojitokeza kupiga kura wakati wa Uchaguzi jambo linaloipunguzia Kura za Ushindi Chama hicho.
🙏
1