Tanzania Investment Centre (TIC)
January 20, 2025 at 09:01 AM
Fursa za Uwekezaji Morogoro: Kilimo cha Viungo(spices) na Viwanda vya Thamani📍
Mkoa wa Morogoro, ni wenye ardhi yenye rutuba na hali nzuri ya hewa kwa kilimo, umeibuka kuwa kitovu cha fursa za uwekezaji, hasa katika sekta ya kilimo cha viungo na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao.
Katika ziara maalum katika miradi ya uwekezaji mkoa wa Morogoro iliyofanyika tarehe 13 Januari 2025, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa, ilitoa wito kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kuchangamkia fursa hizi adimu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mussa Ali Musa, alieleza kuwa mkoa huo, licha ya mafanikio katika kilimo cha mpunga, bado una nafasi kubwa ya kuendeleza kilimo cha viungo(spices) kama karafuu, tangawizi, mdalasini, na mazao mengine ya thamani kubwa.
Wilaya za Gairo, Mvomero, na Kilosa zimeainishwa kuwa na ardhi yenye rutuba inayofaa kwa uzalishaji wa mazao haya, huku zikilenga kuwa kitovu cha uzalishaji kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi.
👍
😢
🙏
3