
Tanzania Investment Centre (TIC)
30.3K subscribers
Verified ChannelAbout Tanzania Investment Centre (TIC)
First point of call for all investors interested to invest in Tanzania. Established to coordinate, encourage, promote and facilitate investment in Tanzania
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

TIC tunashiriki Mkutano wa Kimataifa wa Nchi zinazozalisha Kahawa, unaoendelea katika jijini Dar es Salaam (JINCC) unaifanyika kwa siku mbili tarehe 21 na 22 Februari, 2025. Mkutano huu unawakutanisha viongozi wa nchi mbalimbali, wawekezaji, na wakulima kutoka nchi 25 barani Afrika kwa lengo la kujadili jinsi nchi za Afrika zinavyoweza kushirikiana katika kukuza uzalishaji wa kahawa. TIC tunashiriki katika mkutano na tuna banda katika maonesho kwa lengo la kunadi fursa mbalimbali za uwekezaji kwa ujumla na kilimo cha kahawa. Mkutano huu unatoa fursa ya kubadilishana maarifa na uzoefu kati ya nchi zinazozalisha kahawa, ambapo washiriki wanajadili mbinu bora za kilimo, teknolojia za kisasa, na mikakati ya kuongeza thamani ya zao la kahawa.


https://www.youtube.com/live/cTIkke9VxJg?si=OU9eoTysyi15tutf

Uwekezaji Morogoro๐ Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, tumekutana na kufanya mkutano na wawekezaji katika Mkoa wa Morogoro tarehe 20 Februari 2025. Mkutano huu ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Dkt. Binilith Mahenge, pamoja na wawekezaji na wadau mbalimbali wa sekta ya uwekezaji. Katika Mkutano huu tumejadili njia bora za kukuza na kuimarisha uwekezaji mkoani Morogoro kwa kuzingatia fursa zilizopo. Aidha, mkutano huu ulikuwa ni jukwaa la kubadilishana mawazo kati ya wawekezaji na wadau wengine wa sekta ya uwekezaji kuhusu mikakati bora ya kuendeleza uchumi wa mkoa huu. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, alisema kuwa mkoa huu ni mojawapo ya maeneo yenye fursa nyingi za uwekezaji kutokana na miundombinu bora na maeneo mengi wazi (Open Spaces) yanayowezesha ukuaji wa biashara na uwekezaji. Akitaja sekta za uwekezaji, Mhe. Malima alisisitiza kuwa sekta ya Utalii, Ujenzi, Kilimo, na Madini zinahitaji uwekezaji mkubwa zaidi ili kuzalisha ajira na kuendeleza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla. Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Dkt. Binilith Mahenge, alieleza kuwa Morogoro imeendelea kuimarika katika sekta ya uwekezaji. Katika mwaka 2024, Morogoro ilishika nafasi ya tano kitaifa kwa ukubwa wa uwekezaji, ikiwa na thamani ya Dola za Kimarekani milioni 447.5.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Gilead Teri, akizingumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita leo tarehe 27 Februari, 2025, katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.


Kuelekea Maadhimisho ya Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuelezea Mafanikio na Mwelekeo, Februari 27, 2025.
