Tanzania Investment Centre (TIC)
Tanzania Investment Centre (TIC)
January 20, 2025 at 08:34 PM
Mwanza📍 20 Januari 2025 – Dkt. Bilinith Mahenge, Mwenyekiti wa Bodi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIc) ameipongeza kampuni ya Big Best kwa uamuzi wake wa kuwekeza Tanzania, akisema kuwa, “Uamuzi wenu wa kuwekeza hapa ni muhimu, na tutahakikisha mazingira ya uwekezaji yanaimarishwa ili kufanikisha mradi huu wa kimkakati.” Kauli hiyo alitoa mapema leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Mwanza, ikiwa ni sehemu ya ziara maalum katika mikoa ya kanda ya ziwa. Ziara hii inayoratibiwa na TIC inalenga kutathmini utekelezaji wa miradi mbalimbali. Ziara hiyo inahusisha mikoa mitano ya Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga na Tabora. Lengo kuu ni kujua maendeleo ya miradi inayotekelezwa, kuona changamoto zinazojitokeza, na kujenga mikakati ya kuboresha utekelezaji wa miradi hiyo ili kuleta faida kwa taifa na wananchi.
👍 🙏 ❤️ 😂 😢 7

Comments