Tanzania Investment Centre (TIC)
January 22, 2025 at 08:43 PM
📍GEITA
TIC yaendelea na ziara Kanda ya Ziwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Binilith Mahenge, ameendelea na ziara yake ya kuhamasisha uwekezaji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Katika ziara hiyo, Dkt. Mahenge ametembelea mgodi wa Mwamba na hospitali ya Waja iliyopo mkoani Geita.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Mahenge alisisitiza dhamira ya TIC ya kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuwahamasisha wawekezaji wa ndani kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi. Alisema kuwa sera za uwekezaji za Tanzania zinalenga kuleta mabadiliko makubwa kwa sekta mbalimbali za uchumi kwa kuwapa wawekezaji wa ndani nafasi za kipekee za kunufaika.
“Tumefanikiwa kuwahamasisha wawekezaji wa ndani, na kwa mwaka 2024, idadi ya wawekezaji wa ndani imeongezeka ikilinganishwa na wawekezaji wa nje. Tunaendelea kuwahimiza Watanzania kwamba TIC ni chombo chao, na kuna faida nyingi wanazoweza kupata, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa baadhi ya kodi,” alisema Dkt. Mahenge.
🇹🇿
🫡
2