
Tanzania Investment Centre (TIC)
February 1, 2025 at 05:23 PM
DODOMA📍
Wananchi wa Dodoma Kunufaika na Uwekezaji kupitia Upanuzi wa Kiwanda cha Mafuta ya Alizeti Cemex
Wananchi wa Dodoma wanaendelea kunufaika na uwekezaji kupitia upanuzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Cemex kilichopo jijini Dodoma. Mradi huu umefikia hatua nzuri, ambapo mashine za kisasa zimewekwa ili kuongeza uwezo wa uzalishaji wa mafuta yenye ubora wa hali ya juu.
Kupitia upanuzi huu, wakazi wa Dodoma wataendelela kunifaika kwa njia mbalimbali, ikiwemo fursa za ajira, ujuzi wa kisasa katika kiwanda hiki, pamoja na wakulima wa mbegu za alizeti kupata soko la uhakika kwa mazao yao.
Dkt. Furges Antony msimamizi mkuu wa mradi alibainisha hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya Maafisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), waliotembelea kiwanda hicho ili kukagua na kutathmini maendeleo ya upanuzi huo.
❤️
👍
🙏
6