Tanzania Investment Centre (TIC)
Tanzania Investment Centre (TIC)
February 5, 2025 at 08:22 PM
TIC inashiriki Mkutano wa Utalii na Uwekezaji unaoendelea katika ukumbi wa Eros Hotel, Nehru Place, Delhi, India. Katika mkutano huo, Kituo cha Uwekezaji (TIC) kinatoa wasilisho kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu uwekezaji wakati wa mikutano ya biashara ya ana kwa ana (B2B). Mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega. Kwa upande wa Tanzania, msafara uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mh. Nkoba Mabula. Wengine walioungana katika msafara huo ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Ephraim Mafuru, Wajumbe wa Bodi pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za Serikali, ikiwemo TIC.
❤️ 👍 😂 😢 4

Comments