
Tanzania Investment Centre (TIC)
February 7, 2025 at 06:56 PM
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) leo kimepokea taarifa ya awali ya upembuzi yakinifu kutoka kwa Kampuni ya FIT GROUP ya nchini Nigeria, yenye lengo la kuwekeza katika sekta ya ujenzi wa majengo ya biashara (Real Estate Project).
Taarifa hiyo imeonesha uwepo wa fursa mbalimbali katika sekta ya ujenzi, na tayari kampuni hiyo imeanza mazungumzo na kampuni na taasisi za kizalendo kwa ajili ya kushirikiana katika kuanzisha miradi mbalimbali jijini Dar es Salaam na Dodoma.
Uwekezaji wa miradi hiyo unatarajiwa kufikia zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 75.
❤️
👍
🫂
😂
7