Tanzania Investment Centre (TIC)
February 14, 2025 at 10:32 AM
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea ugeni wa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Mbelwa Kairuki ambapo amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri.
Katika mazungumzo walijadili namna ya kuendelea kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania nchini Uingereza, kwa kutumia miradi ambayo tayari imeshafanyiwa upembuzi yakinifu.
Mazungumzo haya yamelenga kukuza sekta mbalimbali za uchumi, kuongeza ajira, na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza.