IAA Tanzania
February 8, 2025 at 09:33 AM
IAA YAIBUKA KINARA MASHINDANO YA CYBER CHAMPIONS 2025
Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), kimeng'ara katika Mashindano ya CYBER CHAMPIONS mwaka 2025, yaliyoandaliwa na kuratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Bendera ya IAA imepeperushwa vema na mwanafunzi John Mange, ambaye ameshika nafasi ya pili kati ya wanafunzi 600. Pia, IAA ilifanikiwa kutoa washindi saba (07) katika washindi kumi (10) bora wa mashindano hayo.
Mashindano yameshirikisha Taasisi za Elimu ya juu zaidi ya 40 na yamefanyika jijini Dodoma yakilenga kuibua vipaji, kuimarisha uelewa wa usalama mtandaoni na kuwaandaa vijana kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijiti.
👍
❤️
😮
🙏
7