
Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW)
January 26, 2025 at 06:13 AM
Chuo cha Ustawi wa Jamii chukutanisha wawakilishi wa mashirika ya kitaifa na kimataifa, pamoja na wahadhiri na wanafunzi wa Chuo cha Ustawi Wa Jamii tarehe 24, Januari 2025 Katika kampasi ya Dar es Salaam kujadili mapitio ya mitaala.
Akizungumza katika mkutano huo Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Sotco Komba amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za elimu na wadau wa maendeleo ya jamii ili kuhakikisha mitaala hiyo inakidhi mahitaji ya sasa ya kijamii na soko la ajira.
Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na uboreshaji wa mitaala ili iendane na mabadiliko ya kijamii na teknolojia, kuimarisha mafunzo kwa vitendo kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali, na kukuza matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ufundishaji na kufanyatafiti.
👍
❤️
🙏
12