Radio Maria Tanzania
February 17, 2025 at 12:16 PM
SALA YA KUOMBA HURUMA YA MUNGU
Nakimbilia Huruma yako, Ee Mungu mwenye Huruma, uliye pekee mwema. Ingawa dhiki ni kubwa na makosa yangu ni mengi, naitumainia Huruma yako, kwani Wewe ni Mungu wa Huruma na tangu milele haijasikika kamwe, wala Mbingu wala Nchi hazikumbuki kuwa uliiacha roho yoyote iliyotumaini Huruma yako.
Ee Mungu wa Huruma, ni wewe tu uwezaye kunihesabia haki. Ni wewe usiyeweza kunikataa nitubupo na kuukaribia Moyo wako wenye Huruma ambao haujamkatalia mtu yeyote hata kama ana dhambi nyingi kiasi gani.
Kwa kuwa Mwanao alinihakikishia:, " Mbingu na Nchi zingetoweka kwa haraka zaidi kuliko Huruma yangu kukataa kuikumbatia roho iliyo na matumaini"
Ee Yesu, Rafiki wa moyo mpweke ulioachwa, Wewe ni bandari yangu. Wewe ni Amani yangu, Wewe ni Wakovu wangu, Wewe ni utulivu wangu wakati wa mapambano na katikati ya bahari ya mashaka.
Wewe ni mwali mwangavu umulikao njia ya MAISHA yangu. Wewe U kila kitu kwa roho iliyo pweke.
Hata roho ikinyamaza, Wewe waijua na kuifahamu. Unajua udhaifu wetu na unatufariji na kutuponya kama mganga mwema, ukituondolea maumivu Ewe uliye stadi wa kazi. Amina
#injilishakaharaka
#mahujajikatikamatumaini
#radiomariatanzania
❤️
🙏
10