
TRT Afrika Swahili
February 17, 2025 at 11:15 AM
Mwishoni mwa juma aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, ameshindwa katika uchaguzi wa Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika nchini Ethiopia.
Hii imempa yeye fursa ya kurudi nyumbani, ambapo anasema kuna “majukumu muhimu” yanayomsubiri.
Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyu mzoefu kushindwa katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa.
Katika safari yake ya kisiasa ya zaidi ya miongo minne, ameshindwa mara tano alipojaribu kugombea urais nchini Kenya, lakini mara nyingi amepata njia ya kupenya mwanasiasa mwenye ushawishi na huwa na mchango mkubwa hata akiwa upande wa upinzani.
Tunaangazia vipindi alivyokuwa kwenye uchaguzi na kupata matokeo ambayo hayakumridhisha.

😂
👍
😢
🙏
9