
TRT Afrika Swahili
11.8K subscribers
Verified ChannelAbout TRT Afrika Swahili
*Afrika kama ilivyo* 🌐 https://www.trtafrika.com/sw Tiktok ▪️ https://www.tiktok.com/@trtafrikasw Facebook ▪️ https://www.facebook.com/trtafrikaSW Youtube ▪️ https://www.youtube.com/@trtafrikasw X ▪️ https://x.com/trtafrikaSW Instagram ▪️ https://www.instagram.com/trtafrikasw
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

Huku mashambulizi kati ya Iran na Israel yakiendelea, dunia imepata hofu kuhusu Iran kuifunga njia kuu ya bahari inayoitwa Hormuz, inayotumika kusaifirisha bidhaa mbalimbali, ikiwemo mafuta ghafi, gesi na hata makontena. https://vt.tiktok.com/ZSkVTXr1f/

Polisi nchini Kenya imejiweka matatani tena baada ya mtu mmoja kupigwa risasi na afisa wa polisi katika maandamano nchini Kenya 17 Juni 2025. Zaidi ya watu 20 wameripotiwa kujeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika sehemu tofauti nchini wakipinga kifo cha mwanablogu Albert Ojwang akiwa chini ya ulinzi wa polisi. https://www.tiktok.com/@trtafrikasw/video/7517304204923342098

Unafahamu kuwa nafasi wa Ayatollah nchini Iran ni ya uwezo mkubwa kuliko hata ile ya rais? Yeye ndiyo mkuu wa nchi, Amiri jeshi mkuu na ndiyo mwenye kauli ya mwisho inapotokea suala la amri, maagizo na sera za nchi katika masuala mbalimbali Mfahamu zaidi⤵️ https://vt.tiktok.com/ZSkpfHC4V/

“Sitaondoka hapa isipokuwa ni kuelekea kufanya hajji” Hujaji mmoja kutoka Libya aliyeachwa na ndege amekuwa gumzo baada ya ndege hiyo iliyomuacha kushindwa kuendelea na safari hadi walipomkubalia kupanda ndege nao kuelekea Saudia https://trt.global/afrika-swahili/article/2e3d0e768ef1

Ni jiji gani la kwanza kufikia idadi ya watu milioni moja Afrika Mashariki?

Kimnyole Arap Turukat alikuwa ni kiongozi wa nne wa kiroho katika jamii ya Wanandi nchini Kenya, mwanzoni mwa miaka ya 1800. Alisifika sana kwa tabiri zake, ambazo kwa kiasi kikubwa zilibadilisha maisha ya Wanandi kutoka bonde la ufa nchini Kenya. https://youtu.be/ejpv5aMpWec

Sikiliza muhtasari wetu wa habari ya siku ya 19 Mei 2025 🎧 Sikiliza hapa: https://www.trt.global/afrika-swahili/audio/d191d5fcfec3


Ni jiji gani la kwanza kufikia idadi ya watu milioni moja Afrika Mashariki?

Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, mapema hii leo amefikishwa katika Mahakama ya Mkazi ya Kisutu iliyopo jijini Dar es Salaam. Lissu anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo la uhaini. Viongozi mbalimbali, kutoka chama chake cha Chadema, pamoja na baadhi ya wanaharakati kutoka nchini Kenya wamehudhuria kesi hiyo. Awali kumekuwa na taarifa za kuzuiwa kuingia nchini Tanzania kwa baadhi ya wanasheria na wanaharakati kutoka Kenya na hatimae kurudishwa nchini mwao. Aliyekuwa waziri wa katiba Kenya Martha Karua pamoja na mawakili wengine walizuiliwa kuingia Tanzania siku ya Jumapili. Jumatatu Jaji Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga na wanaharakati wengine walirudishwa nyumbani. Lakini jaji mwingine mstaafu wa Kenya David Maraga aliruhusiwa kuhudhuria kesi ya Tundu Lissu jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, serikali ya Tanzania, bado haijatoa ufafanuzi wa sakata hilo.


Rais wa Kenya, William Ruto kwa mara nyingine amewakashifu wakosoaji wake hasa wa kisiasa, wanaopinga uongozi wake. Akitoa mfano, alisema wapinzani hao hawana mawazo mbadala ya kukuza uchumi wa nchi.
