
TRT Afrika Swahili
February 27, 2025 at 07:55 AM
🇨🇩 Zaidi ya watu 7,000 wameuawa mashariki mwa DRC tangu Januari huku waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakiteka miji na maeneo kadhaa.
Kambi 90 zimeharibiwa na watu wengine 450,000 kuhama makazi yao, Waziri Mkuu wa DRC Judith Suminwa ameitaja hali hiyo kuwa “ya kutisha,” akihimiza hatua za kimataifa kukomesha vurugu na kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa.

❤️
😢
2