
TRT Afrika Swahili
February 27, 2025 at 09:52 AM
🇸🇴 🇪🇹 Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anafanya ziara nchini Somalia ambapo anakutana na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.
Ikulu ya Somalia imesema ziara hii inaashiria hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Somalia na Ethiopia.
Majadiliano ya viongozi hao yanafanyika huku kukiwa na mvutano kati ya nchi hizo mbili baada makubaliano baina ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland kuiruhusu kutumia bandari itakayowaunganisha na Bahari ya Shamu.

👍
😢
🙏
3