RFI Kiswahili

RFI Kiswahili

214.2K subscribers

Verified Channel
RFI Kiswahili
RFI Kiswahili
February 22, 2025 at 12:12 PM
Uchunguzi kufuatia moto mkubwa ulioshuhudiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) nchini Kenya unaendelea. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya (KAA), moto huo ulitokea kwenye eneo la nyasi linalozunguka uwanja huo. KAA imeeleza kuwa moto huo haukuathiri miundombinu muhimu wala shughuli za kawaida za uwanja wa ndege, na ratiba za ndege zinaendelea kama kawaida. Hii si mara ya kwanza kwa JKIA kukumbwa na tukio la moto. Mnamo Agosti 7, 2013, moto mkubwa ulizuka katika uwanja huo, na kusababisha kusitishwa kwa shughuli zote kwa muda.
Image from RFI Kiswahili: Uchunguzi kufuatia moto mkubwa ulioshuhudiwa katika uwanja wa ndege wa...
😢 👍 🙏 ❤️ 😂 😮 18

Comments