
JamiiForums
February 26, 2025 at 06:16 PM
Waziri Kivuli wa Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira, Ndolezo Petro, kutoka #actwazalendo ameitaka Serikali kumuachia huru Katibu wa Umoja wa Walimu wasio na Ajira Tanzania (NETO), Daniel Edger Mkinga, baada ya kudaiwa amekamatwa akiwa Kibaha Miembe Saba (Pwani) Nyumbani kwake
Awali, Makamu Mwenyekiti wa NETO, Agness Mpundi, alisema “Tunaomba Wanasheria wenye mapenzi mema na Shirika la Utetezi wa Haki za Binadamu watusaidie kupata Uhuru wake. NETO sio Chama cha kisiasa, genge la Wahalifu wala haina nia yoyote ovu dhidi ya Amani ya Nchi yetu, adhima kuu ya NETO ni kuomba Ajira za Walimu wa Serikali na kusisitiza kufanyia kazi makala tuliyoiandikia Serikali.”
Soma https://jamii.app/NdolezoOnNETO
😂
👍
🙏
4