
JamiiForums
February 27, 2025 at 05:00 PM
Mkurugenzi wa Uchechemuzi (Twaweza), Annastazia Rugaba amechangia mjadala kwa kusema “Wakati mwingine Uchawa unaharibu Viongozi, wapo wanaoingia wakiwa na nia ya kufanya mabadiliko kweli lakini kwa kuwa tunakuwa na tamaduni ya kuwasifia sana, wanazoea na inapotokea wanahojiwa wanakuwa wakali”
Ameongeza kwa kusema kuwa “Tusipopambana na umasikini itakuwa ngumu sana kuondokana na #uchawa. Viongozi wanajua hilo ndiyo maana wanatamani Machawa waendelee”
Amesema kuwa #uchawa huweza kuzuia Uwajibikaji kwa sababu Watu wenye Uhaba wa rasilimali mara nyingi hujikita zaidi katika kukidhi mahitaji ya msingi kuliko kufuatilia utendaji wa Viongozi

👍
❤️
😂
6